Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Ahmad Dastmalchiyan, katika mazungumzo yake na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, alisema kwamba Sayyid Hassan Nasrallah si kiongozi wa muqawama wa Kiislamu Lebanon pekee, bali ni kielelezo kwa wapenzi wa haki na uhuru wote katika ulimwengu wa Kiislamu na hata ulimwengu wa ubinadamu kwa jumla, alisisitiza: mimi kwa yakini naamini kuwa shahada ya Sayyid Hassan imeifanya Jabhatu’l-Muqawama kuwa hai zaidi na yenye nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa kabla.
Akaendelea kueleza kuwa: Shahidi Nasrallah alikuwa mwana Mapinduzi ya Kiislamu halisi na wa Imam Khomeini, na alikuwa mfuasi wa kweli wa wilayat al-faqih. Mara nyingi katika hotuba zake alisisitiza kwamba kufuata kikamilifu wilayat al-faqih ndio siri ya mafanikio na ushindi mkubwa wa muqawama. Hivyo, uhusiano huu wa kina na wilayat al-faqih ulikuwa miongoni mwa fahari kubwa zake, na aliona ndiyo sababu kuu ya mafanikio ya muqawama mbele ya Uzayuni wa kimataifa.
Dastmalchiyan akaongeza: vilevile tunapaswa kutambua kwamba Shahidi Nasrallah alikuwa shakhsia ya kimaulamaa na mjuzi wa maarifa ya Kiislamu. Alisoma katika hawza za Qom na Najaf, na hasa huko Najaf aliathiriwa mno na fikra tukufu za Shahid Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr. Aidha, nchini Lebanon alichukua msukumo kutoka fikra za Imam Musa al-Sadr na Shahid Chamran.
Alisema: urithi huu wa kielimu na kimaana ulimwezesha kutambua alichokipoteza ndani ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kupata njia mpya ya kupambana na ubeberu wa Kizayuni.
Balozi huyo wa zamani wa Iran nchini Lebanon aliendelea kusema: pale utawala wa Kizayuni ulipoivamia Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah, akiwa pamoja na rafiki yake wa jihadi, Shahid Abbas Moussawi, waliweka msingi wa kiini cha Hizbullah. Tangu mwanzo kabisa, kwa kuchanganya elimu ya dini, mtazamo wa kisiasa na roho ya jihadi, aliweza kuandaa uongozi wa kimuundo ulio imara.
Akaongeza: kwa mtazamo huu, Shahidi Nasrallah hakuwa tu mwanazuoni na mfasiri wa fikra za Kiislamu, bali pia alikuwa kiongozi wa kisiasa, kijeshi na kiusalama, ambaye aliigeuza Hizbullah kuwa harakati kubwa zaidi ya muqawama katika eneo lote.
Dastmalchiyan alibainisha: Sayyid Hassan alikuwa na uchambuzi wa kina na sahihi katika masuala ya kieneo na kimataifa. Pamoja na hayo, alikuwa na uwezo wa juu mno katika usimamizi wa kimuundo na uandaaji wa vikosi vya wananchi. Jumla ya sifa hizi zilimfanya Nasrallah asiwe tu kiongozi wa muqawama Lebanon bila mpinzani, bali pia shakhsia yenye athari kubwa kote ulimwengu wa Kiislamu.
Akaongeza: Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa pia kielelezo cha harakati zote za muqawama; iwe katika ulimwengu wa Kiislamu au miongoni mwa mataifa ya wapenzi wa uhuru nje ya eneo. Leo tunapotazama hotuba za viongozi wa Ansarullah Yemen, tunaona wazi kabisa jinsi walivyoathiriwa na shakhsia na fikra za Sayyid al-Muqawama.
Akasema: tunaamini kwa dhati kuwa shahada yake kwa namna yoyote ile haikuwa mwisho wa njia. Kinyume chake, madhehebu yake leo yako hai zaidi kuliko huko nyuma. Shahidi Nasrallah, kama Shahidi Soleimani na mashahidi wengine wakubwa wa muqawama, kwa damu yao wamejenga shule ya kujitolea, mapambano na uadilifu.
Maoni yako